This archive report was first published on 7 November 2019.
Askofu Allan Kiuna aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa saratani, na kufanya Mkana Mungu Harrison Mumia kusema kwamba Mungu hayupo na kwa hivyo hayupo amponye askofu huyo.
Ingawa Mumia alimtakia Kiuna afueni ya haraka, alisisitiza kuwa Mungu hayupo na kwa hivyo hayupo amponye askofu huyo kutokana na maradhi ya Saratani.
"Askofu Kiuna anaugua saratani, ugonjwa ambao sisi sote twajua hauna tiba, hii ni ishara kuwa maombi hayaponyeshi", Mumia alisema.
Aliongeza kuwa Kiuna amekusanya fedha nyingi kutoka kwa waumini wake ambazo amekuwa akitumia kwa matibabu.
Alisema pia kwamba ni wazi kuwa Mungu hayupo, na kwamba jambo la miujizi ni kitendawili tu, kwani Kiuna anapoteza fedha zake hospitalini badala ya kuombea uponyaji wake.