This archive report was first published on 7 November 2019.
Alhamisi, Novemba 7, 2019, Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa alishambuliwa na vijana wenye hamaki alipofika katika kituo cha kupigia kura cha DC eneo bunge la Kibra.
Barasa alikuwa amefika katika kituo hicho kushuhudia jinsi shughuli za upigaji kura zilivyokuwa zikiendeshwa kabla ya kuvamia.
Alipowashwa, Barasa alikwaruzwa, akazabwa makofi kadhaa na kunyang'anywa kofia na vijana hao waliomtaka aondoke katika kituo hicho mara moja.
Barasa alikuwa akizungumza na mbunge wa Dagoretti Kusini Simba Arati kabla ya kuvamiwa na vijana hao mbele ya kamera.
Arati alituliza hali ya Barasa, lakini hali hiyo haikufaulu, na Barasa akilazimika kuondoka.