This archive report was first published on 7 November 2019.
Boni Khalwale kutimuliwa Kibra na taarifa zingine zilizotamba wiki hii ▷ Kenya News ¶
Alhamisi, Novemba 7, 2019
Seneta wa Kakamega, Boni Khalwale, alizomewa na vijana wenye hamaki wakati alikuwa kwenye harakati ya kukagua zoezi la uchaguzi mdogo Kibra. Vijana hao walimvuruga kwa kuingia katika chumba cha kinara wa ODM, Raila Odinga.
Alhamisi, Novemba 7, 2019, Mchekeshaji Njenga Mswahili alipatikana maiti. Mwili wake ulipatikana eneo la Daforeti South, katika Soko la Ndonyo, na inadaiwa aligongwa na treni.
Alhamisi, Novemba 7, 2019, Mbunge Aisha Jumwa amejipata taabani baada ya maafisa wa upelelezi kutambua kuwa mamilioni ya pesa za Hazina ya Serikali Kuu ya Kustawisha Maeneobunge (CDF), za Serikali ya Kaunti ya Kilifi zilitumwa katika akaunti zake za kibinafsi.
Alhamisi, Novemba 7, 2019, Mwaniaji wa Chama cha Jubilee kwenye uchaguzi mdogo ulioanza alfajiri ya Alhamisi, Novemba 7 eneo la Kibra, McDonald Mariga hakupiga kura. Hii ni kwa kuwa mchezaji soka huyo wa zamani amesajiliwa kupiga kura eneo la Starehe jijini Nairobi.
Alhamisi, Novemba 7, 2019, Utata unaomzunguka Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu huenda ni kidonda ndugu ambacho hakitapona karibuni. Hii ni baada ya kundi la wanaharakati linalojiita "Okoa Kiambu" kuwasilisha barua katika bunge la kaunti hiyo ili kufanikisha mchakato wa kumng'atua.
Alhamisi, Novemba 7, 2019, Polisi Kibra waliwatia mbaroni watu wawili wanaodaiwa kuhusika katika ununuaji wa kura. Wawili hao walikamatwa huku uchaguzi mdogo ukiendelea ambapo wagombea 24 wanatoana kijasho.
Alhamisi, Novemba 4, 2019, Shirika la Kitaifa la Takwimu (KNBS) lilitoa matokeo ya idadi ya watu nchini. Shirika hili lilitoa matokeo ya idadi ya watu nchini siku ya Jumatatu, Novemba 4, na kufichua kuwa idadi ya Wakenya kwa sasa ni 47,564296 milioni.
Alhamisi, Novemba 7, 2019, Rais mstaafu Daniel Moi aliondoka hospitali siku ya Alhamisi, Novemba 7, ambako alikuwa amelazwa juma moja lililopita. Moi ambaye hali yake ya afya ilikuwa imezua mdahalao mitandaoni alilazwa hospitalini Oktoba 28 baada ya hali yake ya afya kudorora.
Alhamisi, Novemba 4, 2019, Jaji Mkuu David Maraga ameapaa kuwa hatajiuzulu hivi karibuni licha ya kunyanyaswa kuhusu fedha chache za bajeti alizopatiwa na serikali kuu. Akizungumza na wanahabari Jumatat, Novemba 4, Maraga alisema kupunguza bajeti ya idara ya mahakama imetatiza michakato yote ya mahakama.
Alhamisi, Novemba 6, 2019, Kilo mia moja za dawa ya kulevya aina ya cocaine ziliharibiwa Jumatano, Novemba 6 katika makao makuu ya DCI iliyoko barabara ya Kiambu kaunti ya Nairobi. Dawa hiyo yenye thamani ya takriban KSh 598 milioni iliteketezwa katika maabara ya afisi hizo.