This archive report was first published on 7 November 2019.
Upigaji kura wa uchaguzi mdogo Kibra ulianza 6am Alhamisi, Novemba 7, baada ya miezi miwili ya kupiga kampeni nzito.
Uchaguzi huo umewavutia wapigakura 24, ambao wameanza kupiga kura katika vituo 183 vilivyo na vifaa vya kielektroniki vya KIEMS.
Monica Okoth, mke wa marehemu mbunge wa eneo hilo Ken Okoth, alipiga kura yake Shule ya Kibera Primary.
Wapigakura waliosajiliwa wanatambuliwa kupitia mfumo wa kielekroniki kabla ya kuruhusiwa kupiga kura.
Kiti cha Kibra kilitangazwa kuwa wazi kufuatia kifo cha mbunge Ken Okoth kilichotokea Ijumaa, Julai 26, baada ya kuugua muda mrefu.
Uchaguzi huo umewavutia wapigakura 118,276 ambao walisajiliwa rasmi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.