This archive report was first published on 6 November 2019.
Shughuli za mtihani wa kitaifa katika shule ya binafsi ya Milimani, kaunti ya Kisii, zilitatizika baada ya watahiniwa 16 kususia mtihani ulioanza rasmi Jumanne, Oktoba 4, 2019.
Watahiniwa hao walikosa kufika shuleni kufanya mtihani wa KCSE siku ya tatu, Oktoba 4, 2019, huku watu 11 wakikamatwa kwa kujifanya watahiniwa wa mtihani katika shule hiyo.
Waziri wa Elimu, George Magoha, aliitembelea shule hiyo Jumatano, Oktoba 6, 2019, baada ya kufahamishwa kuhusu kisa hicho.
Magoha alitoa onyo kali kwa wale watakaopatikana wakiiba mtihani, akidai watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Uchunguzi tayari umeanzishwa ili kujua ni kilichowafanya watahiniwa hao 16 kususia mtihani.