This archive report was first published on 5 November 2019.
Polisi mmoja alikuwa na majeraha mabaya baada ya kuruka nje ya dirisha la chumba chake cha kulala akiota usiku katika kituo cha polisi cha Nanyuki, eneo la Laikipia Mashariki.
Aliyetambulika kama Harrison Karagu alikuwa na majeraha mabaya ya kukatwa katwa mikononi na miguuni baada ya kuanguka mita tatu kutoka katika chumba chake cha kulala.
Alisema aliruka nje ya dirisha hilo mwendo wa saa nne usiku kutokana na ndoto ya kuogofya, kulingana na taarifa ya K24 Digital.
Polisi huyo alikimbizwa hospitalini na majirani zake ambao waligutushwa kutokana na tukio hilo.
Maafisa wa trafiki wakiwa kazini. Picha: Citizen.