This archive report was first published on 5 November 2019.
Mtahiniwa wa KCSE wa shule ya upili ya wasichana ya Ngata kaunti ya Nakuru alikataa kufanya mtihani wa KCSE 2019, adai kuwa hakuwa amejiandaa vilivyo.
Mwanafunzi huyo aliwaelezea wasimamizi wa mtihani huo kwamba alijifungua mtoto wake wa kwanza miezi mitatu iliyopita na hajakuwa na wakati wa kujifungua mtoto wake.
Juhudi za kumshawishi mwanafunzi huyo huufanya mtihani huo haujafaulu, huku akisisitiza kuwa atajisajili upya kwa mtihani huo mwaka wa 2020.
Mtihani wa KCSE ulianza rasmi Jumanne, Novemba 4, 2019, huku watahiniwa 699,745 wakitarajiwa kuufanya mtihani huo.
Akithibitisha kisa hicho, naibu kamishna wa kaunti ya Nakuru, Julius Kavita aliaambia wanahabari wa K24 kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ashawasiliana na wakuu wa elimu kuhusiana na uamuzi wake.