This archive report was first published on 5 November 2019.
Wiki kadhaa baada ya Benki ya KCB kukiweka kiwanda cha Mumias chini ya mrasimu, hali iliyopo sasa ni kubwa kuliko shubiri.
Msingi wa hali hii ni kwamba msimamizi mpya aliyefaa kufika Jumatatu, Novemba 4, hakufika ilivyotarajiwa kuchukua hatamu.
Barua rasmi iliyotumiwa kwa wafanyakazi wote inasema kuwa kandarasi zimefutwa na malipo yatatolewa kwa mujibu wa sheria.
Wafanyakazi wa kiwanda hicho wamepigwa kalamu na kufutwa kwa wajibu wao.
Uhaba wa kifedha katika kiwanda hicho ni mkubwa sana, na wakulima na wafanyakazi wakikidai mamilioni ya pesa.
Uchunguzi wa serikali kufufua kiwanda hicho kwa muda mrefu umegonga mwamba, huku wanasiasa wakitoa kauli kinzani.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.