This archive report was first published on 5 November 2019.
Benki Kuu ya Uganda imejitokeza kumuokoa mwanamume ambaye bunda lake la noti lilichomeka na kushindwa kutumika.
Benki hiyo sasa imemuomba mwanamume huyo ambaye alijatambulisha kama Ugaman01 kupeleka pesa hizo katika benki iliyoko karibu ili kuweza kubadilishwa.
Benki hiyo ilimuarifu kuwa huenda noti hizo zikabadilishwa lakini anatakiwa kutimiza baadhi ya masharti.
"Hizi zinaweza kubadilishwa kwa noti mpya, tafadhali peleka katika matawi yetu kati ya saa 9 asubuhi - mchana, Jumatatu - Ijumaa. Matawi yetu yako jijini Kampala, Gulu, Mbarara, Fort Portal, Jinja, Mbale, Arua, Kabale na Masaka," ilijibu benki hiyo.
Benki Kuu ya Uganda ilimjibu kwa kuingilia kati, kwa kusema kuwa anatakiwa kutimiza masharti yafuatayo: saini moja ya gavana au katibu wa benki, nambari moja ya kutambuliwa na nambari moja ya siri, na kuafikia thuluthi mbili ya kipimo chake cha kawaida.