This archive report was first published on 3 November 2019.
Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria ameonya kuwa uwezekano wa machafuko ya baada ya uchaguzi 2022 ni kubwa, kutokana na mivutano iliyopo kuhusu msitu wa Mau.
Alisema hili Jumapili, Novemba 3, 2019, wakati alituma ombi kwa Mwenyezi Mungu kuihurumie Kenya ili isikabiliwe na machafuko mengine.
"Tulikosea Mungu 1991/92. Mungu akatusamehea lakini tena tukakosea 2007/2008. Mungu alitusamehea tena lakini sifikiri atatupa msamaha wa tatu 2022," Kuria alisema.
Aliongeza, "Hatuna Nguvu Yesu. Bila wewe hii safari hatuwezi. Enda nasi bwana."
Alisema hili wakati wa kujipatia pabaya baada ya kutakiwa kufika mbele ya DCI kuandikisha ripoti kwa madai ya kuwachochea wakazi.
Seneta wa Kericho Aaron Cheruiyot alisema serikali imewasukuma sana na huenda ikawalazimu kufanya jambo fulani.
"Tumesema tunataka heshima yetu, na hii vitisho yenu sisi tumechoka nayo. Mmetusukuma na imefikia mahali, itakuwa ni kama umefungia paka kwa nyumba, utaichapa lakini ikipenduka ata wewe utakiona cha mtema kuni," alisema seneta huyo.