Skip to main content

Magavana wa Kitui na Machakos Wamuunga Mkono Imran Okoth Kwenye Uchaguzi wa Kibra

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 2 November 2019.

Magavana wa Kitui na Machakos Wamuunga Mkono Imran Okoth Kwenye Uchaguzi wa Kibra

Magavana wa Kitui Charity Ngilu na Machakos Alfred Mutua wameunga mkono mgombea wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) katika uchaguzi mdogo wa Kibra, Benard Imran Okoth.

Waliandaa mkutano wao Jaramogi Odinga Foundation eneo la Upper Hill jijini Nairobi Jumamosi, Novemba 2, 2019.

Wakisema kuwa ni wakati wa wanasiasa kuweka tofauti zao kando kwa manufaa ya Wakenya umewadia.

"Rais Uhuru Kenyatta na Raila wamekubaliana kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kuleta maendeleo nchini. Hata hivyo, kuna watu fulani humu serikali ambao wanawarudisha nyuma kwa kujihusisha na ufisadi. Kama viongozi kutoka Ukambani tumeamua kumuunga mkono Imran na ODM," alisema Mutua.

Ngilu na Mutua wajumuika na Raila kumuunga mkono Imran.

Wakati uo huo, alivishambulia vyama vingine vya siasa kwa kukosa kufuata utaratibu wa kuwateua wagombea wao katika eneo hilo na badala yake kufuata njia ya mkato kuwachagua.

"Hii tabia ya kuwateua viongozi na kuwashurutisha wananchi kuwachagua ni sharti ikome. Wananchi wanajua kiongozi yule ambaye wanamtaka na nina imani kwamba uchaguzi huu wa Kibra utabainisha matakwa ya wananchi," aliongeza.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →