Skip to main content

Makueni: Kalameni Agura Ibada ya Kununulia Pasta Gari

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 1 November 2019.

Barobaro aliyekuwa akishiriki katika kanisa moja mtaa wa Kibwezi, kaunti ya Makueni, alizua kioja baada ya kukataa kuchanga hela za kununulia gari.

Alisema hana gari moja na hakuwezi kutoa pesa zake kwa ajili ya kununulia mchungaji gari.

Waumini wenzake walipigwa na butwaa kwa mkristo sampuli yake kutoa matamshi kama hayo kanisani na wakaanza kunong'onezana wakimzomea vikali huku wasema kuwa alikuwa mkono gamu.

Aliondoka na kusema kuwa kamwe hatojihusisha na mradi huo kwani watu wengi kanisani humo walikuwa wanapitia hali ngumu ilhali hawafanyiwi michango.

Alisema kuna wagonjwa wanahitaji pesa za matibabu, mayatima wanahitaji karo, na maskini wanalala njaa, na hakuwezi kuhisi hata siku moja pasta akipendekeza kanisa liwachangie ili wasaidiwe.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →