This archive report was first published on 1 November 2019.
Pwani: Kwa Nini Supu ya Pweza Imekuwa Maarufu? ¶
Wakazi wa Pwani wanaendelea kula supu ya pweza kwa ajili ya manufaa yake ya kijeni, ambayo ina madini ya selenium na virutubisho muhimu ambavyo husaidia kuongeza nguvu za kiume na kuboresha tendo la ndoa.
Utafiti wa sayansi umethibitisha kwamba nyama ya pweza ina virutubisho ambavyo husaidia mwili kujikinga na saratani ya mdomo, utumbo mkubwa, shingo ya uzazi, tumbo, mapafu, na titi.
Wengi wa wanaotumia supu hiyo, wanadai kuwa pweza ana uwezo wa kumfanya mwanamume kuongeza misuli na kumfanya kuwa na umbo nzuri kifuani na mikononi.
Shekhe, Mohamed Salim, ambaye ni mmoja wa wakazi wanaokunywa supu ya pweza, anaunga mkono kauli hiyo. "Ni kweli, jambo hili linatokea na sijui kama ni ikwangu tu lakini ukiinywa tu unapata nguvu za aina fulani zikirejea mwilini na hamu ya kufanya tendo huimarika sana. Pia huchoki unapofanya mambo hayo," alisema Salim.
Halima Chichi mkaaji wa Majengo, Mombasa anakubaliana na manufaa ya pweza katika kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa. Chichi anasema supu ya pweza haiwasaidii wanaume pekee yao bali pia wanawake.
Utafiti wa sayansi pia umethibitisha kwamba unywaji supu ya pweza huongeza mbegu za kiume na hivyo, humwezesha mwanamume kuwa katika nafasi nzuri ya kumpachika mwanamke mimba.