This archive report was first published on 1 November 2019.
Wanahabari wa Citizen Lulu Hassan na Rashid Abdhalla wameonyesha penzi lao kwa kuvalia suti zilizofanana wakati wa kufanya kazi.
Wanahabari hao wamekuwa tamanio kwa wengi ambao wanaazimia kuwa katika ndoa.
Wafuasi wao bila shaka walifurahishwa na mtindo wa kimavazi waliovalia wanahabari hao ambao pia ni wanandoa.
Wanahabari hao wamekuwa wakivalia mavazi yanayofanana mara ya kwanza wakati wa mbio za INEOS, wakati waliivalia sare za michezo wakati mwanariadha Eliud Kipchoge alivunja rekodi ya kukimbia kilomita 42 chini ya muda wa saa mbili.