This archive report was first published on 31 October 2019.
Wakenya waliingia kwenye mtandao na kuelezea wasiwasi wao kuwa huenda kuna kiongozi mkuu ambaye amefunga macho baada ya kikosi kikubwa cha wanajeshi kushuhudiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti za Lee.
Wasiwasi huo ulisababishwa na kuwa chumba hicho ndipo viongozi wakuu wa humu nchini hutuliza wanapoaga kabla ya kufanyiwa mazishi ya hadhi.
Uvumi ulikuwa kwenye mitandao kuwa kuna kiongozi mkubwa ambaye yuko katika hali mbaya hospitalini, lakini upekuzi wa TUKO.co.ke umeonyesha kuwa wanajeshi hao walikuwa kwenye chumba hicho kuupokea mwili wa mwenzao jenerali Duncan Kireri Wachira.
Wachira alifariki mnamo Oktoba 22 na mwili wake kuhifadhiwa Lee.
Wakenya waliingia kwenye mtandao na kuelezea wasiwasi wao kuwa huenda kuna mti mnene ambao umegwa.