This archive report was first published on 29 October 2019.
Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i alijumuika na watahiniwa wa darasa la nane katika shule ya msingi ya Gilgil ambapo alishiriki maombi maalumi kabla ya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane kuanza Oktoba 29, 2019.
Alipofika kaunti ya Nakuru kukagua jinsi shughuli za mitihani zilivyokuwa zikiendesha, Matiang'i alitoa maombi ya kibinafsi kwa watahiniwa wa KCPE.
"Tunamkushukuru Mungu kwa kutubariki na hawa watoto, wanapoaanza kufanya mtihani wao, tunawaombea kila la heri na tuko na uhakikaka kwamba watafaulu," Matiang'i aliomba.
Alipomwomba walimu wanaosimamia mitihani ya kitaifa kote nchini, Matiang'i alitoa imani kwamba shughuli hiyo itafanywa ipasavyo.