Skip to main content

Familia ya Mzee Moi Yakana Madai Kuhusu Hali Yake ya Kiafya

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 29 October 2019.

Familia ya Mzee Moi imewahakikishia kuwa mzee huyo hayuko katika hali mbaya kama ilivyoriporiwa na vyombo vya habari.

Msemaji wa familia hiyo, Lee Njiru, amevitaka vyombo vya habari kuwa makini na taarifa zinazotangaza hasa kuhusiana na hali ya kiafya ya Mzee Moi.

Familia ya Mzee Moi ililazimika kujibu madai kuwa yuko katika hali mbaya baada ya yeye kulazwa katika hospitali ya Nairobi Jumanne, Oktoba 29.

Msemaji wa familia hiyo, Lee Njiru, amesema, "Familia ya Moi haijafurahishwa na taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa na vyombo vya habari, ukweli ni kwamba mzee yuko katika hali njema na anaendelea kupokea matibabu kutoka kwa wataalamu wakiongozi na daktari wake wa kibinafsi David Silverstein."

Haya yanajiri majuma mawili tu baada ya Mzee Moi kulazwa katika hospitali ya Nairobi kwa kile familia ilikitaja kama ukaguzi wa kimatibabu wa kawaida.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →