This archive report was first published on 29 October 2019.
Afisa wa Utawala aliyekamatwa Ijumaa, Oktoba 25 kwa kuhifadhi sare za polisi katika chumba chake eneo la Mihango mtaa wa Kayole amezuiliwa kwa siku nne zaidi.
Afisa huyo aliyetambulika kama David Odhiambo atazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kayole huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
Alisimamishwa kazi kwa muda baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu na mahakama ya Malindi.
Uchunguzi ulianza baada ya makachero kutoka Idara ya Upelelezi kuyafumania makazi yake na kumnasa na bidhaa hizo.
Alinasa bidhaa kama sare za polisi wa Utawala, pingu, kofia, viatu, bendera za polisi na mali nyinginezo.
Uchunguzi uliendelea baada ya afisi ya DCI kuiomba mahakama kumzuilia mshukiwa kwa siku tano.
Alipokubaliwa kwa ombi hilo, mshukiwa atazuiliwa kwa siku nne huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
Atatarajiwa kufikishwa mahakamani Novemba 1.
Maafisa wa polisi wanaohudumu katika kituo cha Kayole walidaiwa kuhusika na uhalifu ambao ulipelekea mfanyibiashara mmoja kupoteza KSh 6 milioni katika chumba cha kukodisha cha kulala.