This archive report was first published on 29 October 2019.
Shule ya St Anne Academy Kajulu, kaunti ya Kisumu, inasemekana kuwasajili wanafunzi werevu pekee na wengine kusajiliwa katika shule jirani kwa ajili ya kuepuka matokeo mabaya.
Wazazi wa shule moja ya kibinafsi kaunti ya Kisumu walizua rabsha baada ya kugundua kuwa watoto wao hawakuwa wamesajiliwa kama watahiniwa wa mtihani wa kitaifa wa KCPE katika shule hiyo.
Wazazi hao walivamia shule hiyo na kutaka kuelezewa kwa kina sababu ya watoto wao kupelekwa shule nyingine bila kufahamishwa.
Shule hiyo iliwasajili wanafunzi werevu pekee, wengine wapelekwa shule jirani.
Wazazi wakiwa na hamaki, walisema kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba watoto wao hawako shuleni, na tulikuwa katika shule hiyo kwa ajili ya kuwaombea watahiniwa wa KCPE, hakukuwa na dalili ya wao kuenda kufanyia mtihani katika shule nyingine.