Skip to main content

Afya yako: Jinsi ya kuendelea kuwa na afya bora wakati wa ujauzito

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 29 October 2019.

Ujauzito ni kazi kwa mwili

Mwanamke mjamzito anahitaji kusaidiwa kufanya kazi hasa zinazoweza kuwa nzito na katika kutekeleza majukumu yake; hii ina maana anahitaji muda mwingi kupumzika na miguu yake inafaa kuwa juu mara kadhaa kwa siku. Kulea ujauzito ni kazi kwa mwili; mwili unahitaji kupumzika.

Chakula cha kutosha

Wakati mwanamke mjamzito anailea mimba yake, ni bora kula chakula cha kutosha chenye virutubishi vinavyofaa. Chakula hicho ni lazima kuwa na mchanganyiko wa protini, mboga, matunda, na wanga. Kumbuka mama ni lazima kula chakula cha kutosha yeye na mwanawe.

Epuka matumizi ya bidhaa hatari

Wakati mwanamke mjamzito anailea mimba yake, ni bora kuepuka vitu vinavyoweza kuwa hatari mwilini kama vile pombe, sigara na dawa za kulevya. Sigara na tumbaku huathiri mapafu ya mama na vinaweza kusabisha saratani na hata kifo. Pia moshi unaweza kusababisha mtoto kuzaliwa kabla ya muda wake au akiwa na uzito mdogo sana, au akiwa amekwisha kufa.

Epuka kukutana na wagonjwa

Mwanamke mjamzito kila mara ni lazima kuepukana na magonjwa kwa kuwa kuugua wakati wa ujauzito ni taabu kubwa. Ugonjwa unaweza kusababisha taabu kubwa katika kula, na kutokula chakula cha kutosha humunyima mwanamke mjamzito nguvu. La busara hapa ni kuepuka kukutana na wagonjwa ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa magonjwa.

Makala yameandikwa na Daktari Ali Hassan, daktari binafsi, Nairobi.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →