This archive report was first published on 29 October 2019.
Mshukiwa Mkuu wa Mauaji ya Tob Cohen Aachiliwa Kwa Dhamana ¶
Mahakama Kuu jijini Nairobi ilimwachilia huru Peter Karanja, mshukiwa mkuu wa mauaji ya Tob Cohen, kwa dhamana ya KSh 4 milioni au KSh 2 milioni. Karanja, pamoja na mkewe Sarah Wairimu, alikuwa akikumbana na mashtaka ya mauaji.
Jaji Daniel Ogembo alitoa uamuzi huo mnamo Jumanne, Oktoba 29, 2019. Ogembo alisema kuwa mahakama ina haki ya kuwachilia washukiwa kwa dhamana, kwa kuwa kosa kikuu kinalingana na kosa kikuu cha maisha.
Jaji Ogembo alidai kuwa mahakama inaweza kumnyima mshukiwa dhamna endapo upande wa mashtaka una sababu za kuridhisha za mtuhumiwa kuendelea kuzuiliwa. Hata hivyo, alamuonya mshukiwa kutovuruga uchunguzi katika njia yeyote, ikiwemo kuwasiliana na mashahidi au watu wengine wanaohusika na kesi hiyo.
Karanja alikabithiwa dhamana baada ya Wairimu kukabithiwa dhamana sawia na yake na mahakama hiyo. Wawili hao wanatuhumiwa kwa kupanga njama ya kumuua Cohen pamoja na usaidizi wa watu wengine.
Mwili wa Tob Cohen ulipatikana imetupwa katika tanki ya ardhini siku 40 baada ya kupotea. Kesi hiyo inaendelea.