This archive report was first published on 29 October 2019.
Rais Uhuru na Ruto Wataka Watahiniwa wa KCPE Kila La Heri ¶
Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wameongoza taifa kwa kuwatakia watahiniwa wa darasa la nane katika Mtihani wa Kitaifa wa Shule za Msingi (KCPE) uliofungua Jumanne, Oktoba 29, 2019.
Watahiniwa hao wamekuwa wakijitahidi kufanya vizuri katika mtihani huo, na rais Uhuru na Ruto wamehimiza kujiepusha na udanganyifu wa mtihani na kutumia kile walichofunzwa darasani.
"Maombi yangu ni kuwatakia kila la heri watahiniwa wote watakaofanya mtihani wa KCPE na KCSE. Kama nilivyowambia, mtihani sio mwisho wa maisha lakini hatua katika ndoto zenyu. Walimu wote, wazazi na Wakenya kwa jumla wako pamoja nanyi katoka kipindi hiki," alisema rais Uhuru.
Rais Uhuru pia aliongeza kuwa serikali yake imejitolea kuhakikisha kuwa watahiniwa wote wanapata nafasi kuendeleza masomo yao katika Shule ya Upili, chuo kikuu, chuo cha elimu na pia shule ya kiufundi (TVET).
"Ninawaamni na pia najua mumepewa elimu ya kutosha na habari kuhusu kibarua kinachowasubiri. Juhudi zote na pia kujitolea ili kuhakikisha kuwa munafaulu," aliongeza rais Uhuru.
Naibu wa rais William Ruto aliwatakia watahiniwa heri njema katika mtihani huo wa kitaifa akiwa na imani kuwa watafaulu.