This archive report was first published on 28 October 2019.
Naibu Rais William Ruto amekabiliwa na maswali mengi baada ya Mbunge wa Jubilee Sylvanus Osoro kusema kuwa ni mwizi mkarimu ambaye anaiba fedha za umma na kisha anazitumia pamoja na wafuasi wake.
Osoro alisema Ruto ni mwizi ambaye anaibisha fedha za umma na kisha anazitumia pamoja na wafuasi wake.
Alisema Ruto yuko na fedha nyingi ambazo zinaweza gharamia kampeni kubwa na ghali.
Osoro alisema Ruto sio mchoyo na huwa tayari kushiriki fedha zake na mashabiki.
"Amejiandaa vema, na unavyojua, uchaguzi wowote lazima ugharimike ipasavyo, sisi humkamua ng;ombe na huyu ng;ombe hutoa maziwa mengi mno," Osoro alisema.
Aliongeza, "Iwapo hujawahi iba fedha za umma, basi utatoa wapi pesa utakazotumia ukifanya kampeni?, unahudhuria tu mazishi ila haufiki katika hafla za michango kanisani, na kama ni kuhusu wizi wa fedha za umma, basi ni vema kuwa yule mwizi anayeiba kiasi kidogo kisha anapatia wafuasi wake kiwango kikubwa," Osoro aliongeza.
Ruto alikuwa amehudhuria hafla ya mchango katika kanisa la SDA ambapo alitoa KSh 1.5 milioni na kiasi kingine kisichojulikana katika parokia ya Gekano.