Skip to main content

Mwalimu na Ukuaji wa Kiswahili

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 28 October 2019.

Wakati wa kuzungumza kuhusu ukuaji wa lugha ya Kiswahili, ni muhimu kuzingatia jukumu la mwalimu katika kuendeleza lugha hii. Kwa kuwa Kiswahili ni lugha ya Kiafrika, ni muhimu kwa mwalimu kujitahidi kuwafunza wanafunzi wake kwa njia ifaayo ili lugha hii izidi kuenea zaidi kote duniani.

Walimu wa somo la Kiswahili kote duniani, kuanzia shule za chekechea hadi vyuo vikuu, huwaathiri wanafunzi katika kupenda au kuchukia lugha ya Kiswahili. Ikiwa mwalimu atafunza tu kwa lengo la bora kufunza bila shaka naye mwanafunzi atasoma bora kusoma. Hili linafanya Kiswahili kufa kifo cha madharau.

Wasemavyo husema, ni heri kuwa mwalimu bora si bora mwalimu. Kwa hivyo ni jukumu la mwalimu wa Kiswahili kuhakikisha anaathiri wanafunzi wake kwa njia ifaayo ili lugha hii izidi kuenea zaidi kote duniani. Kumbuka Kiswahili ndio fimbo ya Mwafrika tukitumie.

Titus Sakwa, mwalimu, mwandishi, na mhakiki wa Kiswahili, anasema kwamba mwalimu wa Kiswahili anafaa kuwa kilelelezo na kigezo katika jamii. Afanye wanajamii wakipende Kiswahili na kukitukuza kila wakati.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →