This archive report was first published on 26 October 2019.
Sherehe za Mashujaa Dei zilifanyika mwaka huu huko Mombasa, ambapo risasi moja ilipatikana karibu na bustani ya Mama Ngina.
Polisi walisema risasi hiyo ni hatari kubwa sana kwani ina uwezo wa kuruka kwa hadi mita 3218 kulingana na bunduki iliyotumika.
Wasiwasi umeibuka kuhusu usalama wa Rais Kenyatta baada ya risasi kupatikana karibu na alipokuwa ameketi wakati wa Mashujaa.
Polisi mjini Likoni wamedai risasi hiyo ilikuwa imetumiwa na washukiwa watatu wa ugaidi waliouawa katika mtaa wa mabanda wa Majengo Mapya wiki tatu kabla ya sherehe za Mashujaa kufanyika.
"Kwa sababu risasi ilipatikana, inamaanisha kuna kilichotumika kuitupa," kachero aliambia Daily Nation Oktoba 26.