This archive report was first published on 26 October 2019.
Published on October 26, 2019, Bernie Sanders, mgombea wa urais wa Marekani, ameapa kuhalalisha matumizi ya bangi nchini Marekani baada ya kuchaguliwa kuwa rais.
Alisema atahakikisha utumiaji wa bangi umehalalishwa kwa muda wa siku 100 baada ya kunyakua wadhifa huo.
"Leo ninatangaza mpango wangu, nitahakikisha nimehalalisha bangi ila kwa njia ipasayo, na kusaidia jamii ambazo zimeathirika na utumiaji mbaya wa dawa za kulevya," alisema Sanders.
Madai haya ya Sanders yanatokea wakati viongozi wa Marekani wanaotaka matumizi ya bangi kuhalalishwa kwa minajili ya dawa.
Itakumbukwa kuwa marehemu Ken Okoth alikuwa amewasilisha mswada bungeni akitaka bangi ihalalishwe.