Skip to main content

Wafuasi wa DP Ruto Wapinga BBI Iwapo Itapendekeza Rais Achaguliwe na Bunge

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 25 October 2019.

Wafuasi wa DP Ruto Wapinga BBI Iwapo Itapendekeza Rais Achaguliwe na Bunge

Wafuasi wa DP Ruto wamesema watapinga BBI ikiwa itapendekeza rais achaguliwe na bunge. Wanasiasa wanaoegemea upande wa DP Ruto wameahidi kupinga vikali ripoti ya BBI ikifika bungeni.

Naibu Rais William Ruto alizindua chuo anuwai cha Wanga katika eneo la Mumias Kaunti ya Kakamega, ambapo siasa zilishamiri.

Wakiongozwa na mbunge Bejamin Washiali, kundi la wanasiasa wanaoegemea upande wa DP Ruto liliahidi kupinga vikali ripoti ya BBI ikifika bungeni.

Washiali alisema wanasubiri mapendekezo ya jopo la BBI na litaona kivumbi iwapo kuna mapendekezo kama vile rais kuchaguliwe na bunge.

"Ripoti ya BBI bado ni uvumi kwa sababu bado haijakabidhiwa Rais na kiongozi wa ODM... lakini uvumi unasema inataka wabunge wawe wakichagua rais. Hatutakubaki hilo na Wakenya wataipinga," Washiali alisema.

Seneta wa Kakamega Bonny Khalwale alisema atungamkono BBI kwa sababu imegharimu nchi shilingi bilioni 10, lakini atakuwa tayari kumfanya kampeni ya kuipinga ikiwa itapendekeza kupanua uongozi wa nchi.

"Tutaungamkono BBI kwa sababu imegharimu nchi shilingi bilioni 10. Tutaisoma kwenye maeneo ya biashara na tuwaeleze Wakenya yaliyomo ndio kila mtu aelewe ipasavyo. Lakini iwapo inapania kupanua uongozi wa nchi, basi nitaongoza kampeni za kuipinga," alisema Khalwale.

Wanasiasa wanaoegemea upande wa DP Ruto wameahidi kupinga vikali ripoti ya BBI ikifika bungeni.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →