Skip to main content

Spika Elachi Arudi Afisini Kwa Kishindo, Amsimamisha Kazi Karani wa Bunge

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 25 October 2019.

Spika Beatrice Elachi amerejea afisini kwa kishindo baada ya kuwa nje kwa mwaka mzima. Tayari, siku chache baada ya kurejea afisini, Elachi amemtuma nyumbani karani wa bunge kwa madai ya kukosa kuripoti kazini.

Spika Elachi alisema karani huyo hajakuwa akifika kazini na pia kwenye mikutano ya bodi, na kwa hivyo amemtuma nyumbani kwa likizo la mwezi mmoja ili kuruhusu uchunguzi kufanywa dhidi yake.

"Bodi imekubali kumpa karani Jacob Ngwele likizo la lazima kwa siku 30 kwa kukosakufika kwenye mikutano ya bodi na pia kazini kama anavyohitajika kikatiba," Elachi alisema.

Ngwele atapata mshahara wake kikamilifu wakati wa kipindi hicho cha uchunguzi, lakini atahitaji kujiepushe na kufika kwenye bunge katika kipindi hicho cha mwezi mmoja mpaka uchunguzi ukamilike.

Elachi aliongoza mkutano wa bodi ya bunge hilo na alisema wanachama walikubaliana kwa pamoja kumtuma nyumbani karani Jacod Ngwele kwa kile walisema ni kukosa kufika kazini.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →