This archive report was first published on 24 October 2019.
Seneti ya Kenya iliyopitia kesi ya kumtimua gavana wa Taita Taveta Granton Samboja iliyowasilishwa na mawakilishi wa wadi wa kaunti hiyo, ilifutilia mbali hoja hiyo.
Hoja hiyo ilikuwa ni kwamba gavana Samboja ana uongozi mbaya, na kwa hivyo, anapaswa kutimuliwa afisini.
Walakini, baada ya kuzikiliza hoja hiyo, kamati ya bunge la seneti iling'amua kuwa madai yaliotolewa na mawakilishi hao dhidi ya Samboja yalikuwa dhaifu zaidi.
Spika wa seneti Ken Lusaka alisema uamuzi uliofanywa na kamati hiyo ni tosha na hakuna kura nyingine ya maoni itapigwa ili kumtimua Samboja.
Uamuzi huu ulikuwa ni kufuatia kesi iliyofanyika na mawakilishi wa wadi wa Taita Taveta, ambao walipiga kura ya kutokuwa na imani naye wakidai kuwa ana uongozi mbaya.
Seneti ya Kenya iliyopitia kesi hiyo, ilisema kuwa hoja hiyo ilikuwa ni dhaifu na hakuna msingi.