This archive report was first published on 23 October 2019.
Idara ya utabiri wa hali ya anga ilionya kuhusu mvua kubwa itakayosababisha mafuriko makubwa katika maeneo kadhaa ya nchi.
Wakazi wa mikoa ya Pwani, Magharibi, Kusini Mashariki, Kaskani Mashariki na mkoa wa Kati pamoja na Nairobi watashuhudia mvua yenye milimita 20 kwa muda wa saa 24 kuanzia Jumatano Oktoba 23.
Maeneo kadhaa ya nchi tayari yanashuhudia mvua kubwa tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba.
Madereva pia wameonywa dhidi ya kuendesha magari kwenye barabara zilizofurika maji.
Idara hiyo ilionya kuhusu mafuriko makubwa ambayo yatashuhudiwa kufuatia mvua hiyo kubwa.