This archive report was first published on 23 October 2019.
Sammary Cherotich, mkewe wa mwanariadha Asbel Kiprop, ameonesha dalili za kuendelea baada ya kumtema mumewe bingwa wa mbio za mita 1,500.
Cherotich alipiga ujumbe kwenye ukurasa wake wa Facebook na kusema kuwa kwa sasa ameposwa na jamaa aliyemtambua kama Kelvin Busienei.
Maisha ya Kiprop yamekumbwa na utata tangu alipopigwa marufuku kushiriki riadha na IAAF kufuatia madai ya kutumia dawa za kusisimua misuli.
Cherotich alisema kuwa juhudi za kurejesha uridhiano baina yao kuishi kama mume na mke hazijafaulu.
Wakati wa kipindi hicho, Kiprop alipigwa marufuku kwa kupatikana mwilini na chembechembe za dawa zilizopigwa marufuku na Shirikisho la Riadha (IAAF).
Alipokonywa mataji aliyopokea kati ya Novemba 2017 na Februari 2018, Kiprop alikuwa ameshikilia hana hatia dhidi ya madai hayo na hata kumuomba mkewe msamaha.
Cherotich alisema mwaka 2018, "Asbel amesongwa na mawazo na anahitaji ushauri wa dharura. Eakenya wanastahili kusimama naye jinsi walivyofanya alipoiletea nchi sifa. Simtetei kwa kuwa yeye ni mume wangu ila ni kwa kuwa najua ana kipawa."