Skip to main content

Fisi Waripotiwa Kuvamia Msibani Usiku wa Manane, Wawajeruhi Watu 2

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 23 October 2019.

Usiku wa Jumatatu, Oktoba 22, walikuwa wakijiandaa kupumzika baada ya kumaliza mazishi katika kijiji cha Kasabunga wilayani Bunda mkoani Mara.

Walipokuwa wakijiandaa kulala, fisi walivamia nyumba iliyokuwa na msiba, na kuwajeruhi watu wawili.

Watu hao wawili, David Robert na Bi. Elizabeth Mgeta (60), walikimbizwa na kulazwa katika Hospitali ya Misheni Kibara.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa uvamizi huo ulitokea saa 6 usiku wakati waombolezaji walipokuwa wanajiandaa kulala baada ya kumaliza mazishi.

Idadi ya fisi waliovamia kijiji cha Kasabunga wilayani Bunda mkoani Mara na kuwajeruhi watu 2 bado haijulikani.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →