Skip to main content

Jombi ahamia kwa kipusa kuhepa kelele za mke

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 22 October 2019.

Umbea mtaani unasema kuwa jombi na mkewe walikuwa na ndoa iliyojaa furaha hadi juzi ambapo mambo yalianza kuchacha baada ya jamaa kuonja asali ya nje.

Alipendezwa na kipusa mmoja wa eneo hilo na alipomrushia mistari, kipusa aliingia boksi.

Alipagawishwa kwa mitindo ya kipekee ya mahaba ya mwanadada huyo.

Aliporejea kwake, mkewe alimkemea vikali mbele ya majirani na kumwambia kuwa hatampa nafasi tena ya kuchovya asali yake.

"Wewe ni mtu bure sana! Badala ya kujiinua kiuchumi unajipeleka kwa kisura anayetamani tu hela zako. Hakuna uhusiano tena kati yangu na wewe, ni hii nyumba tu tutatumia pamoja. Hata haki yako ya ndoa hutawahi kuipata," mama aliwaka.

Jamaa ambaye alikuwa na hamaki kwa kuaibishwa aliingia chumbani na kusanya virago kabla ya kumuaga mkewe na kumwabia kuwa alikuwa anaelekea kule atapata raha.

Alimpasha mama huku akiwa ameshika begi ya nguo mikononi.

"Naona ni heri nikuondokee ili nisife hapa kwa mawazo nawe ukae kwa utulivu," jamaa alimpasha mama.

Alipokuona hivyo, mama alianza kulia akimsihi asiondoke huku akiahidi kuwa atabadili mienendo yake ya kumpigia kelele mara kwa mara na badala yake kutafuta njia mwafaka ya kusuluhisha mizozo yao.

Alipokuwa na hamaki kwa kuaibishwa, jamaa alikaa ngumu na kuamua kwenda zake.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →