This archive report was first published on 21 October 2019.
Polisi walilazimisha wakazi Likoni kuoga kinyesi Siku ya Mashujaa ¶
Sherehe za Siku ya Mashujaa zilifanyika kwa usalama wa kutosha kwenye Bustani ya Mama Ngina Waterfront Mombasa, Jumapili, Oktoba 20, 2019.
Wakazi wa eneo la Likoni, Senti Kumi, Majengo Mapya, na Dudus walikuwa wakipitia udhalimu wa jeshi la polisi wakati wa sherehe hizo.
Wanajeshi hao walikuwa wametumwa kuhakikisha hamna msongamano wa magari na vilevile kutibua njama za utatizaji usalama zilizokuwa zimedaiwa zingetokea.
Wanadaiwa kuwa, baadhi ya wakazi walipitia udhalimu wa polisi kwa kupigwa na kuhangaishwa. Hata baadhi yao walilazimishwa kuogelea kwenye vinyesi bila ya kosa.
Wanajeshi hao walitumia bunduki zao kunipiga na kunicaraza makofi. Mimi na mchumba wangu walitulazimisha kukaa kwenye kinyesi, alisema Moses Juma, mmoja wa waliopitia unyama huo.
Salim Matano, ambaye alikuwa na mchumba wake, naye pia alifanyiwa unyama alipokuwa akielekea bustani ya Mama Ngina kutokea eneo la Likoni.
Matano alilazimishwa kuvua nguo huku mchumba wake akitizama kwa uoga na kutoamini kilichokuwa kikiendelea.
Wakazi wa eneo hilo walishuhudia ukatili wa maafisa wa usalama wakati wa sherehe za Siku ya Mashujaa.