This archive report was first published on 21 October 2019.
Sehemu ya tatu ya makala yetu inahusisha jukumu la wazazi katika ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili. Kwa mujibu wa wazazi wengi, wanaohusika katika maisha ya mtoto, wazazi ni kiungo na mhimili mkuu katika maisha ya mtoto. Wazazi hufuata au hutaka kufuata nyendo na maneno ya wazazi wao, na ikiwa mzazi atamwambia mwanawe kuwa kitu au jambo fulani ni zuri au baya, mtoto atafuata.
Wazazi wanachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili. Utapata kuwa asilimia kubwa ya wazazi huwahimiza watoto wao na hata kuwaambia kuwa Kiswahili si lugha ambayo haiwezi kuwapeleka popote. Mara si moja utasikia wazazi wengi wakiwasiliana au kuzungumza nao katika Kiingereza zaidi.
Wazazi na hata mwalimu yafaa ajue na amweleze mwanawe kuwa lugha ya Kiswahili ni kama lugha nyingine na aijue na ajivunie kwayo kwani ndio fimbo ya Mwafrika. Si kwamba lugha ya Kiingereza ndio lugha ya ustaarabu au uungwana. Ifahamike nguo ya kuazima mara zote haisetiri uchi na mja mcha asili haachi asili akiacha asili hana akili. Kiswahili ndio fimbo ya Mwafrika tuitumie.
Titus Sakwa, mwalimu, mwandishi, na mhakiki wa Kiswahili, anasema, "Kiswahili ndio fimbo ya Mwafrika tuitumie."