Skip to main content

Murkomen, Kipkorir inaibuka katika majibizano baada ya Kipchoge kushtaki NRG

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 19 October 2019.

Seneta wa Elgeyo Marakwet, Kipchumba Murkomen, amejikuta katika majibizano makali baada ya kudai kuwa wakili Donald Kipkorir alimpotosha mwanariadha Eliud Kipchoge kukishtaki kituo cha NRG kwa kutumia jina lake kujinufaisha.

Ujumbe huo ulimgadhabisha Kipkorir ambaye alimshambulia kiongozi wa wengi katika seneti na kumuonya dhidi ya kuingilia yayiyomhusu au achukue hatua ya kukiwakilisha kituo hicho.

"Don, sikujua kwamba ni wewe ulimpotosha Kipchoge. Hata hivyo nahisi suala hili lingetatuliwa nje ya mahakama. Kijijini mwangu kuna kibanda kinachotambulika kama Serena kinachouza chai na mandazi. Sitarajii hoteli ya Serena kuwashtaki mahakamani," Seneta Murkomen alisema.

Uchunguzi huo ulianza mnamo Oktoba 19, 2019, baada ya Kipkorir kuwatumia wasimamizi wa kituo hicho barua ya malalamishi kutoka kwa mteja wake.

Wakili wa Kipkorir alirejea na kumsuta seneta huyo kwa kuchukulia masuala ya makampuni au watu binafsi kutumia majina ya wengine kujijengea umaarufu bila uzito.

"Seneta, naomba tuheshimiane kikazi...Iwapo mteja wangu angehisi wewe ni wakili bora zaidi basi angekupa kazi. Kila mtu ashike shughuli yake. Naomba uwawakilishe NRG basi kisha tutaona matokeo," Kipkorir alijibu.

Uchunguzi huo ulikuwa na mawakili wengine na Wakenya waliijitokeza kutoa maoni yao kuhusiana na suala hilo.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →