Skip to main content

Uganda: Rais Museveni Amtaja Bobi Wine Kuwa Adui Nambari Moja

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 18 October 2019.

Uhasama wa kisiasa kati ya Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni na mbunge Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, unaendelea kushuhudiwa nchini humo.

Ikiongea na BBC, Museveni alisema kuwa Bobi Wine ni adui wa maendeleo ya Uganda kwa kutaka wawekezaji wasiingie nchini humo.

Alisema, "Bobi Wine alienda Marekani na kusema kuwa waekezaji hawafai kuja kuwekeza hapa. Hilo linamaanisha yeye ni adui wa maendeleo Uganda," alisema.

Alisema pia kuwa Bobi Wine anawachochea wawekezaji kutowekeza nchini Uganda.

Alisema kuwa mbunge huyo amekuwa msumbufu na ndio sababu hata baadhi ya hafla za miziki yake zimepigwa marufuku.

Wine aliingia mbungeni mwaka wa 2017 kufuatia uchaguzi mdogo ambao alishinda na kuanzia wakati huo amekuwa akimkoa vikali Museveni.

Alisema kuwa bado atasalia mamlakani huku akitarajia kushinda uchaguzi ujao wa mwaka wa 2021.

Published on October 18, 2019, at 2:37 PM EAT.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →