This archive report was first published on 18 October 2019.
Wanamuziki Diamond Platinumz na Tanasha Donna wamekuwa wakijaliwa mtoto wa kiume tangu Oktoba 2, 2019, tarehe ambayo pia mwanamuziki huyo alizaliwa.
Wapenzi hao bado hawajatangaza rasmi jina la mwana wao.
Awali, Tanasha alikuwa amesema hataweka picha za mwanawe mitandaoni kwa hofu kuwa mahasidi wake huenda wakamfanyia maovu.
Walakini, picha ya mtoto huyo sasa imesambaa kwenye mitandao ya kijamii na bila shaka malaika huyo anavutia sana.
Hiyo ni baada ya Diamond kuchapisha mitandaoni picha ya mtoto huyo ila alikuwa ameficha uso wake.
Tanasha na Diamond wamechumbiana kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa baada ya msanii huyo kuachana na mkewe Zari Hassan ambaye walikuwa wamejaliwa watoto 2 kwa pamoja.