This archive report was first published on 17 October 2019.
Nyota wa Manchester City Sergio Aguero alihusika katika ajali ya gari wakati alikuwa akielekea mazoezini siku ya Jumatano, Oktoba 16, 2019.
Aguero alikuwa akiendesha gari lake lenye thamani ya KSh 20 milioni (Pauni 150,000) aina ya LUMMA CLR SV Range Rover Sport wakati wa ajali hiyo.
Staa huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa bahati nzuri alinusurika kwa kutopata majeraha yoyote huku picha za zinazoonyesha kupondeka kwa gari lake zikisambaa.
Sky Sports inadokezea kuwa Aguero aliripoti kwa CFA - City Football Academy, pamoja na kikosi cha City lakini hakufanyiwa uchunguzi na kikosi cha matibabu cha klabu hiyo.
"Tunaelewa hajapata jeraha baada ya kuhusika kwa ajali ndogo ya gari, tumeambiwa aligongesha gari leo asubuhi," mwanahabari wa Sky Sports David Gorrido alinukuliwa akisema.