This archive report was first published on 16 October 2019.
Seneti ya Kenya imechaguliwa kuchunguza madai ya kutimuliwa kwa Gavana Granton Samboja baada ya Bunge la Kaunti ya Taita Taveta kupitisha hoja ya kutokuwa na imani naye.
Madai hayo yamepewa kwa sababu ya matumizi mabaya ya mamlaka, kulipotosha bunge la kaunti, ubadhirifu wa fedha za kaunti kinyume cha sharia kuhusu fedha ya 2012, na kuwa na matamshi ya uchochezi.
Samboja ni gavana wa nne anayekabiliwa na hoja ya kutimuliwa mamlakani, baada ya bunge la kaunti kupitisha hoja ya kutokuwa na imani naye.
Samboja alikuwa amewasilisha kesi mahakamani ya kupinga kutimuliwa kwake na waakilishi wa kaunti, wiki iliyopita.
Seneta wa Siaya James Orengo alisema kwamba Bunge la Seneti halina habari kuhusu kuwasilishwa kwa idhini ya mahakama ya kuzuia kuendelea na majadiliano kuhusu kutimuliwa kwa Samboja na bunge la kaunti.