This archive report was first published on 16 October 2019.
Polisi waliokuwa wakishika doria kwenye barabara kuu ya Nairobi-Mombasa Jumanne, Oktoba 15, 2019, walipatwa na mshangao baada ya kunasa basi la kanisa likiwa linasafirisha bangi.
Basinisi hilo lilikuwa limesafirisha waombolezaji kutoka Kilifi kwenda Homa Bay na wakati wa kurudi likapakiwa na bangi hiyo.
Polisi walisema walanguzi wa dawa hizo walikuwa wamejifanya wajanja kwa kuzificha pamoja na omena katika kujaribu kuwafunga macho maafisa wa polisi.
"Walitaka harufu ya omena kuficha uovu wao lakini hawakujua polisi walikuwa macho," aliongeza OCPD wa Voi Bernastein Shali.
Shali alisema basi hilo ni la kanisa la PEFA na lilikuwa limebeba mamia ya misokoto ya bangi.
"Lilipatikana na misokoto 230 ya bangi ambayo inakisiwa kuwa ya takriban shilingi elfu 46. Dereva wake na watu wengine wawili wamekamatwa," Shali alisema.