Skip to main content

Mabaki ya Miili ya Familia Zilizoangamia Ndege ya Ethiopian Airlines

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 14 October 2019.

Mabaki ya Miili ya Familia Zilizoangamia Ndege ya Ethiopian Airlines

Familia za walioangamia kwenye mkasa wa ndege ya shirika la Ethiopian Airlines zilipokea mabaki ya miili yao Jumatatau, Oktoba 14, 2019, katika Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) nchini Kenya.

Ukumbusho wa wafu ulifanyika katika uwanja huo wa JKIA kuwakumbuka waliofariki dunia kwenye kasa huo uliotikisa dunia nzima.

Abiria walioangamia walikuwa ni raia wa mataifa 35 tofauti, huku idadi kubwa ikiwa ya Wakenya.

Wengine walioangamia kwenye mkasa huo wa ndege ya Boeing 737-800MAX iliyokuwa safarini kuelekea Nairobi walitokea: Canada (18), Misri (6), Ethiopia (9), Ufaransa (7), Marekani (8), Uholanzi (5), Slovakia (4), Uswidi (3), China (8) na Uingereza (7).

Hispania, Israel, Morocco na Poland kila moja zilikuwa na abiria 2, huku Ubelgiji, Indonesia, Ireland, Mozambique, Norway, Saudi, Sudan, Somalia, Serbia, Togo, Uganda, Yemeni, Nepal, Nigeria wakiwa na raia mmoja mmoja.

Uchunguzi wa DNA ulichukua miezi sita kukamilika, na kufanya familia zisafiri miezi kadhaa iliyopita kwenda Addis Ababa, Ethiopia kuchukuliwa sampo za DNA ili kusaidia katika kuitambua miili ya wapendwa wao.

Wakati wa kufanya uchunguzi wa DNA, ilichukua muda mrefu kukamilisha kwa sababu ya jinsi miili ilivyoharibika na ugumu wa kufanya vipimo hivyo bila ya makosa.

Wakati huo huo, familia sita kutoka Kenya zimeishtaki kampuni kubwa ya Marekani inayounda ndege aina ya Boeing kufuatia mkasa huo.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →