Skip to main content

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Feri Bakari Gowa Atakusuluhisha Taarifa DCI

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 14 October 2019.

Uchunguzi umekuwa ukifanywa kubaini chanzo cha ajali ya feri kwenye kivuko cha Likoni ambapo mama na mwanawe walipoteza maisha yao.

Uchunguzi huo umesababisha mkurugenzi mkuu wa shirika la Feri Bakari Gowa kuwa na wajibu wa kuandikisha taarifa kufuatia ajali hiyo.

Upelelezi wa polisi mjini Mombasa umesema kuwa uchunguzi umekuwa ukifanywa kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Benjamin Rotich, kamanda mkuu wa polisi kata ndogo ya kaunti ya Likoni, amesema kuwa Gowa atahitaji kuandikisha taarifa yake wakati ufaao kuhusiana na mkasa huo uliotokea Septemba 29.

Rotich amesema kuwa wana shauriana na mashirika husika ya upelelezi na kwa hivyo hawajatolea tarehe kamili kwa kuandikisha taarifa.

Wakati wa kujibu swali kuhusu taarifa yake, Gowa amesema kuwa hajafahamishwa kuhusu yeye kuandikisha taarifa DCI, lakini yuko tayari kufanya hivyo atapohitajika.

Utepetevu wa Gowa katika shirika lake limesababisha baadhi ya Wakenya kuitaka ajiuzulu.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →