Skip to main content

Familia ya Mariam yakanusha madai kuwa alirudisha gari nyuma akiwa ferini ▷ Kenya News

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 13 October 2019.

Familia ya Mariam yakanusha madai kuwa alirudisha gari nyuma akiwa ferini

Mama Mariam Kighenda na mwanawe Amanda walifariki baada ya gari lao kutumbukia baharini mnamo Septemba 29, 2019, wakati wa kusafiri kwenye feri ya Likoni.

Shirika la feri lilikuwa limedai kuwa Mariam alirudisha gari nyuma na kuanguka majini, lakini familia yake imekanusha madai hayo.

Mumewe wa Mariam, John Wambua, alisema kuwa gari lilikuwa kwenye ngia ya kuegesha na breki ya mkononi ilikuwa imewekwa, kwa hivyo sio wazi kama gari hilo lilirudi nyuma na kutumbukia baharini.

Wanajeshi wa majini wakishirikiana na wapiga mbizi kutoka nchini Afrika kusini walihakikisha kuwa gari pamoja na miili iliyotoka majini ilipolewa Ijumaa, Oktoba 11, 2019.

Uchunguzi wa DCI ulianzishwa kuhusiana na mkasa huo, na tayari makachero wamehaji watu watano ambao walikuwa kwenye feri wakati wa mkasa.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →