Skip to main content

Mauti ya Mariam Kighenda na Mwanawe Amanda Mutheu Baharini: Mume Wao Anasimulia

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 13 October 2019.

Mauti ya Mariam Kighenda na Mwanawe Amanda Mutheu Baharini

Familia ya Mariam Kighenda na Amanda Mutheu inaendelea kuomboleza vifo vya wawili hao huku shughuli za mazishi zikiendelea baada ya miili yao kuopolewa baharini Ijumaa Oktoba 11.

Wawili hao walizama bahari mnamo Jumapili, Septemba 29, baada ya gari lao kurudi nyuma lilipokuwa kwenye feri katika kivukio cha Likoni na kutumbukia majini.

Alama ya gari linalotumbukia baharini ilipolewa Ijumaa Oktoba 11. Picha: UGC

Alama ya gari linalotumbukia baharini ilipolewa Ijumaa Oktoba 11. Picha: UGC

Alama ya gari linalotumbukia baharini ilipolewa Ijumaa Oktoba 11. Picha: UGC

Mumewe wa Mariam, Kighenda John Wambua, alisimulia jinsi alipata habari za mauti ya familia yake.

"Ilikuwa kama mida ya saa saba hivi wakati ambapo alimaliza shughuli za nyumbani na akachukua kikapu na gari na akaenda shambani Kwale," alisema Wambua.

Wambua alisema kuwa wawili hao walikuwa kwenye mazungumzo hadi wakati wa Mariam na mwanawe Amanda walipokuwa wameabiria feri ya MV Harambee tayari kuvukishwa hadi upande wa pili.

"Kile Wambua hakujua ni kuwa mazungumzo yao wawili wakati huo wa jioni ndiyo yalikuwa ya mwisho," alisema.

Wambua alisema kuwa alipata ujumbe kwenye twitter kuwa kuna gari limetumbukia kwenye bahari, na picha ya gari hilo ilifanana na gari letu kwa hivyo aliamua kumpigia simu.

"Hata hivyo, simu ya mkewe ilikuwa haiingii na ndipo wasiwasi ukamzidi zaidi na kuamua kukimbia kwenye kivukio cha Likoni," alisema.

Wambua alisema kuwa alimpigia lakini alikuwa mteja na si kawaida yake. Ndipo alikimbia kwa feri na ndipo wakaniarifu mkasa uliofanyika.

Wambua amebaki na mtoto wao mvulana mwenye miaka kumi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →