Skip to main content

Maafisa 10 wa Polisi Wafariki Katika Shambulizi Garissa

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 13 October 2019.

Maafisa 10 wa polisi kutoka kitengo cha General Service Unit (GSU) wamepoteza maisha yao baada ya gari walilokuwa wakisafiria kukanyaga vilipuzi vilivyokuwa vimetegwa barabarani katika kaunti ya Garissa.

Shambulizi hilo lilitokea siku ya Jumamosi jioni, Oktoba 12, katika barabara ya Degoh huku maafisa hao wakilinda mpaka wa Kenya na Somalia.

Inspekta Genarali Hillary Mutyambai alisema kikosi cha kutoa ulinzi kimetumwa kuwasaka washambulizi hao ambao wanashukiwa kutoka kwa kundi la kigaidi la al-Shaabab.

Utumizi wa magari ya kivita yamesaidia katika kupungua kwa visa hivyo kwani yana uwezo wa kulinda polisi dhidi ya vilipuzi.

Kenya inapania kupokea ndege sita za kivita kutoka Marekanai kufikia Desemba mwaka huu ili kusaidia katika vita vinavyoendelea dhidi ya magaidi.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →