This archive report was first published on 12 October 2019.
Published on October 12, 2019, Eliud Kipchoge amesisimua Wakenya baada ya kufaulu kukimbia kilomita 42 chini na masaa mawili na kuweka rekodi ya kuwa bindamu wa kwanza kuwahi kufanya hivyo.
Wakenya walikuwa wakisubiria matokea ya mtoto wao huku wakishikilia pumzi na ushindi wake ulipokelewa kwa shangwe na mahanjam ya kila aina.
Alimaliza kilomita zote 42 kwa 1:59:40 katika shindano la INEOS 1:59, na viongozi mbali mbali wamemsifia mwanariadha huyo kwa ukakamavu wake na ari ya kujituma kwenye mbio hizo.
Naibu Rais William Ruto na Raila Odinga walikuwa na wakati mzuri kujivunia ushindi wake na kumpa heko moja kwa moja.
Ulimwengu mzima ulimwangazia mwanariadha huyo, na kujizatiti na kuhakikisha kuwa anaweka rekodi hiyo kwenye shindano hilo la INEOS 1:59.