This archive report was first published on 12 October 2019.
MC Jessy aliwasha moto mtandaoni baada ya muigizaji Shix Kapienga kufika kwenye kipindi cha 10/10 Ijumaa Oktoba 11.
Shix Kapienga alikuwa ameibuka kwa kipindi hicho ambacho vijana hunengua viuno kwa midundo ya kisasa.
MC Jessy aliandika, "Najivunia wewe Ghettogirl kila wakati. Endelea kupaa zaidi," kwa Shix Kapienga.
Walimsifu sana binti huyo ambaye aliibuka wakati akiigiza katika kwenye vipindi kama vile Beba Beba.
Walitaka MC Jessy ajitokeze na kumtambua Shix Kapienga kama barafu yake ya roho.
MC Jessy alikuwa amevunja ndoa yake na mkewe, na uvumi wa penzi lao ulichipuka baada ya habari hiyo.