This archive report was first published on 12 October 2019.
Rais Uhuru Kenyatta alituma rambirambi zake kwa familia ya John Wambua ambaye alimpoteza mkewe Mariam Kighenda na mtoto wao Amanda Mutheu baada ya wawili hao kutumbukia baharini Jumamosi, Oktoba 12.
Wawili hao walizama majini baada ya gari lao ambalo lilikuwa katika feri kurudi nyuma na kutumbukia kwenye bahari mnamo Septemba 29.
"Kando na mabadiliko yanayofanywa ili kuimarisha huduma za feri, daraja la Likoni Gate, ujenzi wa barabara ya Dongo-kundu pamoja na ile ya Samburu-Kinango-Kwale itasaidia kumaliza presha katika kuvuka kisiwa cha Mombasa na Pwani Kusini," Rais Kenyatta alisema.
Wanajeshi wa majini wakishirikiana na wapiga mbizi kutoka nchini Afrika kusini ndio ambao waliendeleza zoezi hilo la kuhakikisha gari hilo pamoja na miili imetoka majini.