This archive report was first published on 10 October 2019.
Mvua kubwa ilisababisha maporomoko ya ardhi eneo la Mathioya ¶
Maporomoko ya ardhi yalitokea eneo la Mathioya, kaunti ya Murang'a baada ya kutokea kwa mvua kubwa iliyonyesha. Idara ya hali ya hewa ilisema kuwa baadhi ya mimea ya chai iling'olewa.
Idara hiyo ilionya wakazi wa eneo hilo kuhusu mvua inayotarajiwa na wito kwa wakazi wa maeneo hayo kuhama kwenye maeneo salama ili kuepeuka majanga ambayo huenda yakatokea.
Idara ya hali ya hewa ilisema kuwa eneo hilo limeshuhudia kiasi cha 140mm cha mvua kwa siku tano zilizopita. Licha ya kwamba hamna majeruhi wameripotiwa kuathirika na tukio hilo, waakazi wametakiwa kuwa macho na kuhamia maeneo yaliyo salama ili kuepeuka majanga ambayo huenda yakatokea.
Awali 2018, watu watano walizikwa wangali hai baada ya kutokea maporomoko ya ardhi. Picha: TUKO.co.ke